03 May 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Arusha wmetakiwa kuweka sheria ndogo za kupitisha mifugo
 
2007-05-03 17:50:21
Na Radio One Habari

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Kanali Samwel Ndomba ameziagiza Halmashauri za Wilaya mkoani humo kuweka sheria ndogondogo za njia za kupitisha mifugo ili kudhibiti uharibifu wa barabara unaotokana na tabia ya kupitisha mifugo barabarani.

Kanali Ndomba ametoa agizo hilo wakati wa mkutano wa 21 wa Bodi ya Barabara Mkoa wa Arusha ambao pia umehudhuriwa na Waziri Mkuu na ambaye pia ni Mbunge wa Monduli Mheshimiwa Edward Lowassa.

Kanali Ndomba amesema sheria hizo zitasaidia kuanisha njia za kuvushia mifugo na akataja maeneo yaliyokithiri kwa upitishaji wa mifugo barabarani kuwa ni pamoja na Monduli Juu, Selela na Engaresero yaliyoko katika wilaya ya Monduli pamoja na Engarenanyuki iliyoko Wilayani Arumeru.

Mkuu huyo w Mkoa wa Arusha amezitaka wilaya zote mkoani humo kukomesha uvamizi wa maeneo ya akiba ya barabara hasa sehemu za mijini hasa katika barabara za Arusha hadi Moshi, Arusha hadi Namanga na maeneo ya Mbuada.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.