|
Wachimba mchnga wavamia viwanja 200 vya ujenzi Dodoma
2007-05-02 17:50:14
Na Radio One Habari
Zaidi ya viwanja 200 vilivyopimwa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu kwa ajili ya ujenzi katika maeneo ya Kisasa, Mapinduzi na Mwangaza, vimevamiwa na wachimba mchanga.
Akizungumza na shirika la habari la PST mjini Dodoma, Mkurugenzi wa Miliki Ardhi wa Mamlaka hiyo Bwana Costantino Mofuli amesema viwanja hivyo havifai tena kwa matumizi ya kujenga kutokana na kubaki makorongo makubwa.
Bwana Mofuli amesema mamlaka tayari imeunda kamati ya mazingira yenye wajumbe kutoka Usalama wa raia, manispaa na Idara ya Madini na mamlaka yenyewe ambao watakuwa na jukumu la kulinda maeneo hayo.
Amefafanua kuwa, kamati hiyo imeshaanza kufanya kazi yake na mpaka sasa imekamata malori 11 ya kusomba mchanga.
|