01 May 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Serikali imetetea zoezi la kuwahamisha wafugaji kutoka Bonde la Ihefu
 
2007-05-01 16:52:43
Na Radio One Habari

Serikali imetetea zoezi la kuwahamisha wafugaji kutoka Bonde la Ihefu Mkoani Mbeya kwamba halikufanywa kwa nia ya kuaadhibu bali kuokoa vyanzo vya maji ambayo ni muhimu kwa kufua umeme hapa nchini.

Akizungumza na baadhi ya wafugaji na wanavijiji vya Mbwemkuru, Kiranjeranje na Matandu Wilayani Kilwa, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bwana Said Meck Sadick amewataka wafugaji kuyapuuza maneno hayo ambayo amesema yanalenga kuipaka matope Serikali.

Amesema kitendo cha Serikali kuwatengea wafugaji maeneo mazuri ya kufugia na kilimo pamoja na maandalizi yanayofanywa ya kuwajengea majosho na malambo ya maji ni kielelezo tosha kuwa inawajali na kuwathamini wafugaji.

Hata hivyo amewataka wafugaji kuwa wa kweli katika kutoa idadi sahihi ya mifugo yao ili kuiwezesha Serikali inapoandaa ununuzi wa dawa za mifugo kusiwepo na upungufu.

Aidha amewataka wafugaji walio na mifugo mingi kuuza baadhi ya mifugo kwa lengo la kuboresha maisha yao kwa kujenga nyumba bora na za kudumu na kuondokana na tabia ya kuhamahama kunakofanya watoto wao kukosa elimu.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.