|
Utozaji wa ushuru mara mbili kutolewa ufafanuzi Zbar
2006-07-23 22:53:00
Na Radio One Habari
Serikali ya mapinduzi Zanzibar imeahidi kutoa ufafanuzi juu ya malalamiko ya wafanyabiashjara wa Zanzibar kutozwa ushuru mara mbili na Mamlaka ya Usafiri wa nchi Kavu na Baharini-SUMATRA-.
Ahadi hiyo imetolewa mjini Zanzibar na Waziri Kiongozi, mheshimiwa Shamsi Vuai Nahoidha katika Baraza la Wawakilishi wakati akitoa ufafanuzi juu ya madai ya mamlaka hiyo kufanya kazi Zahodha.
Mheshimiwa Nahodha alilazimika kutoa ahadi hioyo kufuatia hoja ya Mwakilishi wa jimbo la Chambani wa CUF, mheshimiwa Abass Juma Mhunzi aliyezuia kifungu cha bajeti ya Wizara ya Utalii, Biashara na Uwekezaji akitaka maelezo juu ya malalamiko hayo ya wafanyabiashara wa Zanzibar.
Aidha, Waziri Kiongozi ameipa siku tatu wizara hiyo siku tatu kukutana na Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar na taasisi inayolalamikiwa ili kutafuta ufumbuzi kwa kipindi hiki cha mpito kabla ya mazungumzo ya kero za muungano.
Awali, mheshimiwa Mhunzi alidai kero za muungano zipo kwa muda mrefu na wafanyabiashara wa Zanzibar wamekuwa wakipata matatizo na alishauri Baraza la Wawakilishi liunde chombo maalum kulipatia ufumbuzi suala hilo.
|