|
Serikali itatumia sh. bilioni 11 na milioni 200 kwa ajili ya kuboresha usafiri
2006-07-17 14:36:11
Na Radio One Habari
Serikali itatumia shilingi bilioni 11 na milioni 200 kwa ajili ya kuboresha usafiri katika jiji la Dar es Salaam kama mojawapo ya njia za kuondoa msongamano wa magari katika barabara za jiji.
Naibu Waziri wa Miundombinu Mhe. Makongoro Mahanga amesema baadhi ya hatua zinazochukuliwa na serikali ni pamoja na kuanzisha mradi wa mabasi yaendayo kasi, upanuzi na ukarabati wa barabara kuu muhimu za Kilwa, Sam Nujoma na Mandela, utakaoanza hivi karibuni, na kuanzisha usafiri wa majini kwa maeneo yaliyo kandokando ya ufukwe wa bahari.
Amesema hatua nyingine ni kupanua Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kuwa na njia nne kuanzia makutano ya barabara ya Morocco hadi Tegeta.
Mhe. Mahanga alikuwa akijibu swali kuhusu athari za msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam na hatua ambazo serikali inazozichukua kutatua tatizo hilo.
|