16 Jul 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Tanzania na Congo zatiliana saini kuhusu usalama wa ziwa Tanganyika
 
2006-07-16 19:09:47
Na Radio One Habari

Tanzania na Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo zimetiliana saini maazimio saba ya utekelezaji kwa ajili ya kuimarisha usalama wa ziwa Tanganyika baina ya nchi hizo.

Maazimio hayo yamefikiwa katika kikao cha ujirani mwema cha watalaam kutoka nchi hizo kilichofanyika mjini Kigoma.

Katika maazimio hayo wataalamu hao wamekubaliana kuwa hizo kwa kushirikiana ziimarishe ulinzi katika mipaka ya nchi zao kwenye ziwa Tanganyika, kuwabaini wahamiaji haramu na kuwarejesha katika nchi zao.

Wamekubaliana pamoja na mambo mengine, kuwepo utaratibu wa mawasiliano kati ya vyombo vya usalama vya nchi hizi mbili kwa ajili ya kupeana taarifa za matukio na jinsi ya kuona uwezekano wa kuyakabili pale yanapotokea au yanapotaka kutokea na kuwepo na mikutno ya ujirani mwema kuanzia ngazi ya wilaya hadi mkoa kila baada ya miezi mitatu ikiandaliwa kwa kupokezana.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.