16 Jul 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Auwa mkewe baada ya kuzuiwa kupiga mtoto
 
2006-07-16 19:08:16
Na Radio One Habari

Mkazi wa kijiji cha Kanazi wilayani Ngara, mkoani Kagera, Bwana Dedani Yona amemuua mke wake kwa kumpiga na kumkaba shingo baada ya mwanamke huyo kumzuia mumewe kumpiga mtoto wao.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Kanazi, Bwana Michael Efta amemtaja mwanamke aliyeuawa kuwa ni Yudita Dedani na kwamba mauaji hayo yalitokea siku ya Alhamisi saa tatu usiku nyumbani kwa wanandoa hao.

Marehemu ameacha watoto watatu akiwemo mtoto mchanga mwenye umri wa miezi saba.

Dedani Yona pamoja na jirani yake mmoja wanashikiliwa na polisi wilayani Ngara ambapo jirani huyo anaisaidia polisi kwa sababu aliwahi kufika kwenye eneo la tukio wakati ugomvi ukiendelea.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.