|
Shirika la nyumba kujenga maghorofa mikoani
2006-07-16 19:04:39
Na Radio One Habari
Shirika la Nyumba la Taifa linatarajia kumaliza tatizo la uhaba wa nyumba za kupanga nchini kwa kuongeza maghorofa mengine kwa kila mkoa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Bibi Salome Sijaona amesema hayo alipotoa maelezo kwa Rais Jakaya Kikwete mipango mbali mbali ya shirika hilo kwenye uwekaji wa jiwe la msingi kwenye ujenzi wa maghorofa mawili ya shirika hilo yaliyopo katika eneo la Mpwapwa Mafleti Mkoani Dodoma.
Maghorofa hayo yenye ghorofa nne yatakuwa na uwezo wa kuchukua familia 24 na yatagharimu Shilingi Bilioni 1.88 na yatakamilkka mapema Februari mwakani.
Bibi Sijaona amesema shirika lina majengo mengi kwenye maeneo muhimu kati kati ya miji ya nchi, lakini majengo mengi yamechakaa na mengine yamepitwa na wakati na hivyo hayastahili kuwepo katik kati ya mji.
Amesema kutokana na tatizo hilo shirika limewashirikisha wawekezaji wengine wenye uwezo ili kuendeleza maeneo hayo ya kati ya miji kwa kuvunja majengo yaliyopo na kujenga majengo makubwa zaidi.
|