16 Jul 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Waomba taarifa ya tume kuhusu mustakabali wa madini ya Tanzanite
 
2006-07-16 19:03:57
Na Radio One Habari

Wachimbaji wadogo wadogo wa madini katika migodi ya Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara wameiomba Wizara ya Nishati na Madini kutekeleza ahadi ya kuiweka bayana taarifa ya tume ya Jenerali mstaafu Robert Mboma kuhusu mustakabali wa madini ya Tanzanite.

Katibu mkuu wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini mkoani Arusha(AREMA), Bwana Isaya Latema ameliambia shirika la habari la PST kuwa Waziri wa Nishati na Madini Dk.Ibrahim Msabaha wa alitoa ahadi hiyo ya kuweka taarifa hiyo hadharani alipotembelea machimbo hayo mapema mwezi Mei, mwaka huu.

Bwana Latema amesema kutowekwa hadharani kwa taarifa hiyo mpaka sasa kunawasonononesha wachimbaji wadogo wa Tanzanite kwani wanaamini kama ingetangazwa ingekuwa nafasi nzuri ya kumaliza mgogoro wa muda mrefu kati yao na Kampuni ya wawekezaji kutoka Afrika ya Kusini ya TanzaniteOne.

Waziri Mkuu, mheshimiwa Edward Lowassa alitembelea Mererani mapema mwaka huu, ambapo wachimbaji wadogo walitoa malalamiko mbalimbali ukiwemo mgogoro wao na kampuni ya Tanzanite One ambapo Waziri Mkuu aliahidi kumtuma Waziri wa Nishati na Madini kutafuta ufumbuzi wa migogoro ya Mererani

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.