|
Vinara 2 wanaosadikika na matukio utekaji wa magari wamekamatwa
2006-07-12 15:32:45
Na Radio One Habari
Polisi Mkoani Mwanza wamewatia mbaroni watuhumiwa wawili wanaosadikiwa kuwa vinara wa matukio mbalimbali ya utekaji wa magari matika mapori Biharamulo, Bukombe, Katoro na Samina.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Bwana Zelothe Stephen ameiambia PST kuwa watuhumiwa hao waliokuwa wakisakwa kwa muda mrefu walikamatwa katika pori la Samina, lilopo wilayani Geita Mkoani Mwanza.
Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Charles Chacha au Mseti na Fidelis Silvester ambapo baada ya kuwahoji wamesema kuwa wote ni wakazi wa kijiji cha Nyamwanga, wilayani Tarime, Mkoani Mara
Kamanda Stephen amesema kuwa jeshi hilo lilifanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa hao kutokana na taarifa mbalimbali za wasamaria wema na kuwa walikuwa na taarifa zao za kuhusika na matukio ya uporaji na utekaji magari.
|