13 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Arusha yatinga robo fainali
 
2008-05-13 08:49:41
By Jimmy Charles

Timu ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru Warriors, jana wamekata tiketi ya kusonga mbele katika mashindano ya Kombe la Taifa yanayoendelea kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, baada ya kuinyoa Iringa, Ruha Stars, kwa bao 1-0 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja huo.

Ruha Stars ambao walifuzu hatua ya pili ya mashindano hayo baada ya kuinywesha ulanzi Manyara kwa kuifunga mabao 4-1, jana ilishindwa kufurukuta pale walipojikuta wakizamishwa kwa bao hilo pekee katika mchezo huo lililofungwa na Abdalla Juma katika dakika ya 24 na kudumu hadi mwisho wa mchezo huo.

Mfungaji wa bao hilo aliwatoka walinzi wa Iringa Aidan Haule na Omar Mussa katika harakati zake za kufunga bao hilo lililoitoa kimasomaso Arusha, ambayo imeanzia hatua ya pili baada ya kutokuwa na mpinzani katika hatua ya kwanza.

Kwa ushindi huo, Arusha sasa imefuzu kucheza hatua ya robo fainali, ambapo itasubiri kucheza na mshindi wa mechi ya leo kati ya Kagera na Ruvuma.

Mchezaji Mussa Akashi wa Arusha ndiye mchezaji bora katika mchezo huo na aliibuka na kitita cha sh. 50,000.

Katika hatua nyingine kocha mahiri nchini Syllasaid Mziray alijitahidi kuipigia chapuo Iringa na kuipa baadhi ya mbinu ili iibuke na ushindi, lakini maji yalizidi unga baada ya timu hiyo kulowa mbele ya Arusha katika mchezo mkali na wakusisimua.

Mziray akiwa amesimama karibu na aliyekuwa Mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto, alifanya kila jitihada kuhakikisha anapenyeza mbinu ili ziwafikie wachezaji wa Iringa.

Timu ya mkoa wa Arusha inafundishwa na kocha wa zamani wa Simba Madaraka Bendera, wakati ile ya Iringa inafundishwa Swalehe Mollel.

  • SOURCE: Nipashe
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.