13 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

TEFA wapinga kupokonywa ushindi
 
2008-05-13 08:47:28
By Somoe Ng\'itu

Chama cha soka cha mkoa wa Temeke (TEFA) kinapinga kupokonywa ushindi walioupata katika mchezo wake wa hatua ya kwanza dhidi ya mabingwa watetezi, Mbeya katika mashindano ya kuwania kombe la Safari Lager Taifa Cup yanayoendelea kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa TEFA, Athumani Nyamlani alisema jana kuwa wanapinga Mbeya kupewa ushindi kwa sababu wachezaji wanaodaiwa kuwa waliwachezesha kinyume na tataribu walikuwa wamefukuzwa na klabu ya Mtibwa Sugar na barua za kutimuliwa wanazo.

Wachezaji hao ni Sammy Kessy na Rashid Gumbo ambao wote Shirikisho la soka nchini (TFF) linasema kuwa walitoa vibali vya uhamisho vya kimataifa kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.

Nyamlani alisema pia TEFA haikupewa muda wa kujiandaa na utetezi katika kikao cha rufaa kilichofanywa na kamati ya mashindano ya michuano hiyo hivyo hawakutendewa haki.

Alisema pia wanasikitika kuona wachezaji wao wamedhalilishwa kwa kufukuzwa hotelini na kutupiwa vifaa vyao baada ya kutoka mazoezini na kusema kuwa kitendo hicho hakikuwa cha kiungwana huku viongozi wakipewa nakala ya maamuzi ya rufaa juzi jioni.

Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela alisema jana kuwa timu hiyo iliitwa katika kikao hicho na ilishindwa kuhudhuria na hivyo kamati iliendesha kikao na kutoa maamuzi kwa kuzingatia kanuni zilizowekwa.

Mwakalebela alisema kuwa kamati ya mashindano ilishindwa kupitia usajili wa wachezaji kutokana na mikoa kushindwa kuwakilisha usajili wao kwa wakati uliopangwa.

``Temeke ni moja ya mikoa iliyoshindwa kukamilisha usajili na kutokana na hali hiyo na sisi tulihitaji kuona mashindano yanafanyika tuliendesha mashindano kwa kuamini kuwa vyama vya mikoa vingekuwa waaminifu,`` alisema Mwakalebela.

Aliongeza kuwa maamuzi ya kamati hiyo ni ya mwisho na hivyo wataendelea kuitambua Mbeya kuwa ndio timu iliyosonga mbele kwenye mashindano hayo baada ya kukata rufaa katika muda uliotakiwa na kulipa ada ya Sh. 300,000.

Temeke ilifanikiwa kuibuka na ushindi baada ya kuiondoa Mbeya kwa penati 5-3.

Timu hizo zilimaliza dakika 90 zikiwa zimefungana mabao 2-2.

  • SOURCE: Nipashe
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.