Sportsnews |
 |
NAVIGATION |
 |
|
 |
|
|
 |
SEARCH |
 |
|
|
|
 |
SPECIAL |
|
|
 |
|
|
 |
ARCHIVES |
|
|
 |
|
|
 |
|
 |
|
|
|
APR wamuombea Odhiambo
2008-05-13 08:46:40
By Somoe Ng\'itu
Chama cha soka la Rwanda (FERWAFA) kimesema kuwa tayari kimeshatuma barua kwa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya kumuombea kibali cha uhamisho cha kimataifa (ITC) mshambuliaji mpya wa APR, Moses Odhiambo.
Odhiambo ambaye ni Mkenya ameichezea Simba katika msimu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ambayo imemalizika mwezi uliopita na Yanga kufanikiwa kuibuka kuwa mabingwa.
Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Cesar Kalisa alisema kuwa tayari APR wameshakamilisha usajili wa mchezaji huyo na wao kama chama wameshatuma barua kwa TFF kwa ajili ya kupata kibali hicho na kuweza kuitumikia APR.
Kalisa alisema kuwa hata hivyo Odhiambo hataweza kuichezea APR katika msimu wa ligi unaoendelea kutokana na muda wa usajili wa dirisha dogo kuwa umemalizika hivyo ataanza kuitumikia timu yake hiyo katika msimu ujao unaotarajiwa kuanza mapema mwezi Septemba.
Alisema kuwa hivi sasa timu zinaruhusiwa kuanza zoezi la usajili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi ambapo ndio mchezaji huo ameombewa na klabu hiyo yenye mashabiki wengi zaidi nchini Rwanda.
Kalisa alisema kuwa ligi yao inatarajiwa kukamilika mwezi Julai na kuitaja timu ya Atraco ambayo alikuwa anaichezea mshambuliaji wa Simba, Athumani Machupa ndio inaongoza katika msimamo wa ligi na kufuatiwa na APR na wapinzani wao Rayon.Odhiambo ambaye alikuwa nyota katika kikosi cha Simba inadaiwa kuwa ameuzwa kwa kiasi cha Dola za Marekani 10,000.
APR ambayo ndio mabingwa wa soka msimu uliopita ndio itaiwakilisha Rwanda katika mashindano ya Kombe la Kagame ambayo yamepangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 12 hadi 24.
|
|
 |
TODAY |
|
|
----------------------------------------------- |
Editorial |
|
|
----------------------------------------------- |
Business
bits |
|
|
----------------------------------------------- |
|
|
| |
 |
|