12 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Washindi wa bahati nasibu ya TBL wapatikana
 
2008-05-12 08:53:02
By Mwandishi Wetu

Washindi tisa wa droo ya nne ya shindano la ``Kili Time Of Your Life`` linaloendeshwa na Kampuni ya Bia nchini (TBL)limefanyika na washindi wa wiki wamepatikana kwa njia ya bahati nasibu na kujinyakulia mamilioni.

Shindano hili linawawezesha wanywaji wa bia kujipatia fedha za kuwasaidia kuboresha maisha yao.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Oscar Shelukindo aliwataja washindi wa sh. milioni tano kuwa ni Ibrahim Mgawe wa Dar es salaam, Salum Feruzi wa Shinyanga na Patrick George wa Korogwe.

Waliojishindia sh.milioni mbili ni Zawadi Kisima wa Dar es Salaam, Fuledi Maganga wa Mwanza naAlois Msaki wa Singida wakati waliojishindia milioni moja ni Veronica Ngamlagosi wa Dar es salaam, Fortunata Paul wa Mwanza na Ulirick
Njau wa Arusha.

Washindi hao wamepatikana baada ya kuwasilisha fomu ambazo zina magamba matano ya vizibo vya bia ya Kilimanjaro yaliyoandikwa ``Kili time of Your Life`.

Shelukindo alisema kuwa katika shindano hilo, Tanzania imegawanywa kwenye kanda tatu, Kanda ya Kusini kupitia Dar es Salaam, Kanda ya Ziwa kupitia Mwanza na Kaskazini Mashariki kupitia Arusha.

Kanda zote hizi tatu zimeibuka na washindi watano ambapo Mshindi wa 5 na 4 wamejishindia kamera kama kifuta machozi , wa tatu atajinyakulia Sh. milioni moja, wa pili sh. milioni mbili na mshindi wa kwanza atajipatia millioni tano fedha taslimu.

Shindano hili linaendeshwa kwa muda wa wiki nane, ambapo kila wiki millioni 24 zinashindaniwa.

  • SOURCE: Nipashe
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.