11 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Bonite Bottlers yasaidia saruji mifuko 300
 
2008-05-11 11:52:59
Na Victor Kwayu, PST Moshi

Kampuni ya Bonite Bottlers iliyopo Moshi mkoani Kilimanjaro, imetoa msaada wa mifuko 300 ya saruji yenye thamani ya Sh. milioni 4.5, kwa Shule ya Sekondari ya Darajani iliyopo mkoani hapa.

Msaada huo, ulikabidhiwa kwa Mkuu wa shule hiyo, Bw.Thadei Kwayi na Meneja Utumishi na Utawala wa Bonite, Bw.Dominick Urassa, kwa niaba ya Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Limited, Bw.Reginald Mengi.

Bw.Urassa, alisema Bw.Mengi aliguswa na hali iliyokuwa ikiikabili shule hiyo, hususani jengo la ghorofa tatu ambalo ujenzi wake ulikwama.

Alisema kwa hali hiyo, Bw. Mengi alitoa mifuko 300 ya saruji, ili itumike kuendeleza ujenzi wa ghorofa hilo litakalokuwa na madarasa matatu.

``Mengi aliguswa na hali hii na ndio maana ameamua kuwaunga mkono katika jitihada zenu, ametuagiza tulete salaam zake kwenu, kutokana na majukumu mbali mbali yanayomkabili hakuweza kufika hapa leo, lakini pokeeni msaada huu kama mchango wake kwenu,`` alisema Bw. Urassa.

Naye Mkuu wa shule hiyo, Bw.Thadei Kwayi, alisema uongozi wa shule hiyo, Bodi na wanafunzi walipata faraja kutokana na kupata msaada huo.

Bw. Kwayi, alisema uongozi wake ulishakata tamaa kuhusu kuendelea kwa ujenzi wa jengo hilo.

Alisema awali shule hiyo ilianza katika majengo duni yaliyokuwa mabanda ya mifugo na hatimaye kufanyiwa ukarabati mwaka 1999.

  • SOURCE: Nipashe
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.