11 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

TCRA yaandaa maadhimisho ya teknolojia ya Habari na Mawasiliano
 
2008-05-11 11:50:41
Na Joseph Mwendapole

Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), imeandaa maonyesho ya wiki moja ya Teknolojia na Mawasiliano na Habari (TEKNOHAMA), ambayo yanatarajia kuanza kesho jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Profesa John Mkoma, alisema maadhimisho hayo ya siku sita hufanyika duniani kote kila mwezi wa tano wa kila mwaka na kilele huwa tarehe 17 ya mwezi huo.

Alisema lengo la maadhimisho hayo ni kuwafanya wananchi kujua umuhimu wa matumizi ya TEKNOHAMA katika shughuli zao za kila siku.

Alisema lengo ni kuunganisha nguvu na wadau wa sekta hiyo, serikali na taasisi mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya TEKNOHAMA na kuhamasisha matumizi yake.

Profesa Mkoma alisema sekta hiyo imekuwa muhimu katika ukuaji wa uchumi na aliwahamasisha watanzania kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho hayo.

Alisema kutakuwa na maonyesho mbalimbali yanayohusu TAKNOHAMA na mada mbalimbali zitatolewa na wataalamu wa sekta hiyo ili kuwapa wananchi kuelewa mpana kuhusiana na masuala ya teknolojia.

Alisema maudhui ya maadhimisho ya mwaka huu ni `Matumizi ya TEKNOHAMA kwa walemavu na watu wote,`.

Aidha, alitaja watakaoshiriki maadhimisho hayo kuwa ni TCRA, Wizara ya Sayansi, Mawasiliano na Elimu ya Juu, Baraza la Watumiaji wa Mawasiliano, wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi na sekondari na Vyuo Vikuu.

Alisema idadi ya watumiaji wa mtandao Tanzania bado ni ndogo na aliwahamasisha wananchi kujitokeza kuitumia.

Alisema kupitia mtandao wanafunzi na wananchi wa kawaida wanaweza kupata taarifa mbalimbali zenye manufaa kwao.

``Silazima kutumia intaneti kwa mambo machafu, katika mtandao unaweza kupata mambo mazuri ya kuelimisha na unaweza kuitumia kama maktaba yako,``alisema.

  • SOURCE: Nipashe
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.