10 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Boban kutua nchini leo
 
2008-05-10 10:26:59
By Somoe Ng`itu

Kiungo mahiri wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, Haruna Moshi `Boban` anatarajiwa kuwasili nchini leo kujiunga na kambi ya timu hiyo kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya Mauritius ambao umepangwa kufanyika Mei 31, kwenye Uwanja Mpya wa Kisasa uliopo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jana, Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka nchini, TFF, Fredrick Mwakalebela alisema kuwa Boban ambaye anatokea katika klabu ya Muscat FC ya Oman atajiunga katika kambi hiyo pamoja na wachezaji wengine wanaocheza soka ya kulipwa kujiandaa na mchezo huo ambao ni wa kundi A wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za mashindano ya Kombe la Dunia na Kombe la Mataifa ya Afrika za mwaka 2010.

Mwakalebela alisema kuwa baada ya kuwasili kwa mchezaji huyo atakuwa amebakia Erasto Nyoni ambaye anachezea klabu ya Vital O ya Rwanda ambaye bado shirikisho linaendelea kuwasiliana naye ili ajiunge mapema na kambi hiyo.

Awali, kulikuwa na taarifa kuwa Boban tayari alikuwa ameshawasili nchini lakini amechelewa kujiunga na kambi hiyo bila ya kutoa sababu maalumu.

Katika mechi hiyo Stars itamkosa beki wake tegemeo, Shadrack Nsajigwa anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata mwaka jana wakati walipocheza na Burkina Faso.

Wakati huo huo, Stars inaendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala kujiandaa na mchezo wake wa marudiano dhidi ya Uganda, The Cranes, utakaofanyika Mei 17.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Marcio Maximo amesema kuwa majeruhi Abdi Kassim, Uhuru Selemani na Henry Joseph wanaendelea vizuri na hataongeza mchezaji yoyote endapo hawatakuwa wamepona na badala yake nafasi zao zitajazwa na wachezaji wengine walioko katika kikosi hicho.

  • SOURCE: Nipashe
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.