08 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Kondic kutembeza panga leo
 
2008-05-08 09:47:49
By Jimmy Charles

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa hatma ya wachezaji watakaoichezea timu yao katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na mashindano mengine ya kimataifa inatarajiwa kujulikana leo baada ya Kocha Mkuu, Dusan Kondic kuwasilisha mapendekezo katika zoezi la usajili.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Imani Madega alisema kuwa hatma ya wachezaji watakaoachwa na watakaoendelea kuitumikia Yanga itajulikana katika kikao cha leo ambacho kitajadili mapendekezo yaliyotolewa na kocha wao.

Madega alisema kuwa Kamati ya Utendaji ilikuwa kimya ikiwa inasubiri mapendekezo ya kocha mara baada ya kumalizikia kwa Ligi Kuu ambapo wanaamini kuwa atakuwa amelenga katika kuboresha kikosi hicho.

Madega alisema lengo la kumuachia zoezi hilo Kondic ni kufahamu kuwa atakuwa amechagua wachezaji watakaoiletea Yanga manufaa makubwa katika kwa kuzingatia kurekebisha mapungufu yaliyokuwepo ili kuwa na kikosi imara kitakachofanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali na hasa ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika mwakani.

``Masuala yote ya usajili tumemuachia Kondic, tunategemea kuwa kesho (leo) kocha wetu atatuwasilishia mapendekezo yake na mara baada ya kuyawasilisha kwetu tutayafanyia kazi haraka iwezekanavyo,`` alisema Madega.

Aliongeza kuwa Kamati ya usajili ya klabu hiyo inatarajia kuanza kazi hiyo Jumatatu ambapo itazunguka katika maeneo mbalimbali yaliyopendekezwa na kocha ili kuwafuata wachezaji wanaohitajika.

Alisema pia Yanga katika msimu ujao imetenga fedha maalumu kwa ajili ya kukamilisha zoezi la usajili ambapo itakuwa na uwezo wa kumnunua mchezaji itakayemuhitaji kwa gharama yoyote.

``Yanga ni taasisi kubwa, tumejipanga kikamilifu kuhakikisha tunampata mchezaji yeyote atakayehitajiwa na Kondic, hilo linawezekana na wala hatuna wasiwasi nalo,``aliongeza Madega.

Alisema kuwa baadhi ya wachezaji watakaotemwa watafikiriwa kupewa chochote lengo likiwa ni kuujali mchango wao katika kipindi chote walichokuwa ndani ya timu.

  • SOURCE: Nipashe
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.