02 Feb 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Yanga yafanya mauaji
 
2008-02-02 08:45:20
By Onesmo Kapinga

Yanga jana ililipa kisasi kwa Coastal Union baada ya kuikandika mabao 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo wa duru la kwanza uliofanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, Yanga ililowa 1-0 katika mchezo uliopigwa Septemba 26, mwaka jana.

Yanga ikitawala mchezo huo kwa kiasi kikubwa, iliandika bao la kwanza katika dakika yan 45 lililofungwa na Mkenya Maurice Sunguti kwa kichwa baada ya kupata mpira kutoka kwa Credo Mwaipopo aliyepata mpira wa kona iliyochongwa na Athumani Idd.

Vijana hao wa Jangwani wakiendelea kulisakama lango la wapinzani wao, waliandika bao la pili katika dakika ya 58 lililofungwa na Abuu Ramadhani baada ya Fred Mbuna kurusha mpira mrefu uliombabatiza mfungaji na kujaa wavuni kabla ya Jerry Tegete hajafunga jingine katika dakika ya 78 baada ya pasi ya Sunguti aliyewatoka mabeki wa Coastal.

Tegete alifunga tena katika dakika ya 90 kufuatia krosi ya Mrisho Ngassa, huku Coastal Union ikipata pigo jingine katika 60 baada ya mchezaji wao Soud Mtezo kutolewa nje kwa kupewa kadi ya pili ya njano kufuatia kubishana na mwamuzi Pascal Chiganga wa Mara.

Kwa matokeo hayo, Yanga ina pointi sawa na Prisons ya Mbeya iliyopo kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 27, lakini imeizidi Yanga kwa tofauti ya mabao ya kufunga.

Kocha wa Coastal Union, Rashid Shedu alisema kuwa timu yake imefungwa kwa sababu ya kuwa na chipukizi wengi na walimtegemea sana Uhuru Seleman kufunga mabao.

Wakati huohuo, Yosso wa Yanga nao waliibuka na ushindi dhidi ya wenzao wa Ashanti katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja huo kabla ya kuanza pambano la wakubwa.

Yanga:Jackson Chove, Mbuna, Amir Maftaha, Nadir Haroub `Canavaro`, Wisdom Ndlove, Hamis Yussuf, Mwaipopo, Sunguti, Abuu Ramadhani na Athumani Idd.

Coastal Union:Ismail Suma, Ally Ahmed, Msulwa Thabiti, Sadat Salum, William Baswelu, Denis Tasso, Sudi Mtezo, Ally Mkuba, Kudura Maguta, Abdu Said/Uhuru Selemani na William Juma.

  • SOURCE: Nipashe
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.