Sportsnews |
 |
NAVIGATION |
 |
|
 |
|
|
 |
SEARCH |
 |
|
|
|
 |
SPECIAL |
|
|
 |
|
|
 |
ARCHIVES |
|
|
 |
|
|
 |
|
 |
|
|
|
Simba nayo yafanya kweli
2008-02-02 08:44:41
By Jimmy Charles, Morogoro
Timu ya Simba ya Dar es Salaam, jana ilizidi kuonyesha makucha yake katika Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuikandamiza Polisi Morogoro kwa mabao 3-0 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini hapa.
Ikicheza kandanda safi hasa katika kipindi cha pili, Simba ilianza kuandika bao la kwanza dakika tano baada ya kuanza kwa mchezo huo lililofungwa na Athumani Machupa akiunganisha wavuni krosi ya Ulimboka Mwakingwe.
Kipindi cha pili Simba ilicharuka zaidi hasa baada ya kuingia kwa Mussa Hassan `Mgosi` na Julius Mrope waliochukua nafasi za Nassoro Said na Emmanuel Gabriel ambao waliichachafya sana ngome ya Polisi na kusababisha kupatikana kwa bao la pili katika dakika ya 69 lililofungwa na Mohamed Banka baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Polisi.
Simba iliendelea kulisakama lango la wapinzani wake na kufanikiwa kufunga bao la tatu lililowekwa kimiani na Mrope kufuatia krosi safi kutoka kwa Mwakingwe aliyefanya kazi kubwa kabla ya kupiga mpira huo uliomkuta mfungaji.
Kocha wa Polisi Morogoro John Simkoko alisema baada ya mchezo huo kuwa timu yake ilifungwa kutokana na makosa waliyofanya ambayo yalitumiwa vizuri na wachezaji wa Simba kupata mabao hayo.
Naye Jamhuri Kihwelu ambaye ni kocha wa Simba alisema kuwa amefurahishwa sana na mchezo waliocheza wachezaji wake lakini hakuridhishwa na idadi ya mabao waliyofunga kwani alidai kuwa ni machache.
Charles Ngereza anaripoti kutoka Arusha kuwa;timu ya JKT Ruvu jana iliendeleza wimbi la ushindi baada ya kuifunga Kagera Sugar kwa mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Mabao ya JKT yakifungwa na Hussein Bunu katika dakika ya tatu na Amos Migisa katika dakika ya 58, huku lile la Kagera likifungwa na Michael Katende katika dakika ya 78.
Kutoka Dodoma Mary Edward anaripoti kuwa; timu ya Polisi ya huko imeshindwa kutamba baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Manyema katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri.
Bao la wenyeji lilifungwa na Said Bigambo katika dakika ya tano wakati lile la wageni lilipachikwa na Idd Juma katika dakika ya 47.
|
|
 |
TODAY |
|
|
----------------------------------------------- |
Editorial |
|
|
----------------------------------------------- |
Business
bits |
|
|
----------------------------------------------- |
|
|
| |
 |
|