23 Jul 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wakaguzi punguzeni rushwa -Meghji
 
2006-07-23 11:05:58
Na Lucy Lyatuu

Waziri wa fedha, Bi. Zakhia Meghji, amewataka wakaguzi wakuu wa hesabu za serikali kupunguza tatizo la rushwa. Alisema njia moja wapo ya kupunguza tatizo hilo ni kufanya kazi kwa kuzingatia maslahi ya taifa.

Waziri Meghji alisema hayo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Wakaguzi wa hesabu za serikali mjini Bagamoyo jana.

Alisema bado kuna baadhi ya watumishi ambao sio waaminifu na waangalifu katika kutelekeza azma kuu ya wakaguzi wa hesabu za serikali.

’’Lazima kuangalia ni nani anayeathirika inapotokea matumizi mabaya ya fedha za serikali, kwa nafasi zenu zingatieni maslahi ya taifa na sio maslahi yenu binafsi,’’ alisema Waziri Meghji.

Aliongeza kuwa serikali inataka kuona taarifa sahihi zenye kuzingatia viwango na kanuni zinazotakiwa ili kulinufaisha taifa.

Alisema wakaguzi wanatakiwa kutoa taarifa zinazoendana na wakati na sio kufanya udanganyifu wowote.

Waziri Meghji alisema wahusika hao wapatiwe elimu inayokidhi matakwa ya taifa ili kutoa taarifa sahihi na zenye kuboresha taifa ili kutumika kwa ufasaha zaidi.

Aidha, alisema sekta hiyo inatakiwa kuongeza idadi ya wakaguzi wanawake ili kuendana na kasi mpya ari mpya na nguvu mpya.

Alisema hayo kutokana na idadi ya wakaguzi wanawake nchini kuwa wachache kulinganisha na wanaume walio katika sekta hiyo.

Kwa upande wake Kaimu Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Dk. Frank Mhilu, alitoa wito kwa serikali kuimarisha uwajibikaji wa wakaguzi ikiwa ni pamoja na kuwawezesha.

Alisema wakaguzi wengi wanapata maslahi duni kulinganisha na wahasibu wa serikali hali inayosababisha kukosesha watumishi wenye sifa nzuri serikalini.

Dk. Mhilu alisema wakaguzi wengi wana vyeo vya ukaimu miaka mingi hali inayoonyesha hakuna kupandishwa vyeo katika sekta hiyo.

Mkutano huo wa siku moja umewakutanisha wakaguzi wa hesabu za serikali mbalimbali nchini kwa lengo la kuzungumzia ajira na maadili katika utumishi wa umma na majadiliano kuhusiana na ugonjwa wa Ukimwi na magonjwa mengine ya kuambukiza.

  • SOURCE: Nipashe
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.