23 Jul 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Polisi yaua mahabusu akitoroka
 
2006-07-23 11:03:43
Na Thobias Mwanakatwe, PST, Tanga

Mahabusu mmoja aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya mauaji amepigwa risasi na polisi na kufa papo hapo, wakati akijaribu kutoroka akiwa chini ya ulinzi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Bw. Issaya Mngulu, aliiambia PST jana kuwa mahabusu huyo, Athumani Ramadhani Mfundo (37), mkazi wa kijiji cha Kwediamba alipigwa risasi hizo mjini Handeni muda mfupi baada ya kushushwa toka kwenye karandinga, kupelekewa mahakamani.

Mahabusu waliokuwa kwenye karandika hilo walikuwa 29 wakitokea gereza la Handeni kupelekwa mahakamani ambapo kati yao watatu akiwemo marehemu walikuwa wakikabiliwa na kesi ya kumuua Bw.Adamu Athumani.

Bw. Mngulu, alisema mahabusu walipoteremka kwenye karandiga nje ya mahakama, Mfundo alitimiu mbio na kuelekea porini katika msitu wa hifadhi ya Handeni.

Kufutia tukio hilo, baadhi ya askari waliokuwa wakiwalinda mahabusu hao walianza kumfukuza na askari mmoja aliyekuwa na silaha alipiga risasi tatu hewani ili kumtisha Mfundo asimame, lakini aliendelea kutimua mbio na ndipo askari huyo alifyatua risasi na kumjeruhi katika mguu wa kushoto chini ya goti na kusababisha aanguke.

Kamanda Mngulu alisema askari walimkamata na kumpeleka katika hospitali ya wilaya ya Handeni kwa matibabu lakini kutokana na kuvuja damu nyingi alifariki dunia.

  • SOURCE: Nipashe
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.