16 Jul 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Benki ya Dunia imetuona Watanzania
 
2006-07-16 10:38:54
Na Mhariri

Rais wa Benki ya Dunia(WB), Bw.Paul Wolfowtz katika ziara yake nchini wiki hii amekonga nyoyo za Watanzania kutokana na ahadi zake kemkem zilizolenga kupatia ufumbuzi matatizo sugu yanayoikabili Tanzania.

Moja ya ahadi hizo ni kwa taasisi yake kusaidia kutatua tatizo la umeme katika nchi za Arika Mashariki ambazo ni Tanzania, Kenya na Uganda.

Akasema tatizo la umeme ni sugu na limesababisha kushuka kwa uzalishaji kwa nchi hizo. Na kwamba kama halitapatiwa ufumbuzi litazorotesha uchumi wake.

Ahadi hii ya kiongozi huyo wa juu katika vyombo vya fedha duniani, hakika imeleta matumaini mapya kwa nchi yetu kutokana na ukweli kwamba tatizo la umeme sasa ni sugu.

Hivi sasa umeme unatolewa kwa mgao katika maeneo mbalimbali nchini.

Hii imetokana na kukosekana kwa mvua za kutosha hivyo kusababisha upungufu mkubwa wa maji katika mabwana yanayozalisha umeme.

Siyo siri kwamba tatizo hili kwa muda mrefu limeiumiza kichwa serikali ambapo pia hutumia fedha nyingi kuzalisha umeme unaotokana na mafuta.

Matokeo yake mara kwa mara umeme kupatikana kwa mgao, hatua ambayo imeathiri sana uzalishaji viwandani na adha kwa matumizi ya majumbani.

’’Tutaangalia jinsi ya kusaidia tatizo kwa kutafuta vyanzo mbadala vya nishati vitakavyosaidia kuboresha hali hiyo’’, anasema Rais huyo wa WB.

Ila akasisitiza katika ahadi hii kwamba kinachohitajika ni utashi wa viongozi wa nchi zetu katika kutekeleza miradi iliyokusudiwa.

Ni faraja kubwa kwa Watanzania kwamba WB imetuona na kuionyesha nia safi ya kusaidia tatizo hilo la umeme ambalo limezorotoshe uchumi wa nchi yetu kwa muda mrefu sasa.

Isitoshe, hata kufikia dhamira kiongozi huyu kupanga ratiba yake kuzitembelea nchi zetu, ni kiashiria tosha kwamba msaada huo unahitajika ili kuondoa kiu ya wananchi katika kujiletea maendeleo.

Kinachotakiwa, kama alivyosistiza, ni namna ya kutekeleza vizuri miradi itakayolenga kutatua matatizo yetu likiwemo hilo la umeme.

Kwa kuwa tatizo hili la umeme limeathiri uchumi wetu kwa kiwango kikubwa, tunaamini kwamba pindi miradi hiyo iliahidiwa na WB itakapotekelezwa, usimamizi wake nao utakuwa makini ili ilete matunda yaliyokusudiwa.

  • SOURCE: Nipashe
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.