|
Wadau wa mawasiliano kuathimisha siku yao May 17
2008-05-11 19:50:44
Na ITV Habari
Wadau wa mawasiliano wa hapa nchini May 17 mwaka huu wanaungana na wenzao dunani kote kuadhimisha siku ya teknolojia ya habari na mawasiliano huku nchi ikikabiliwa na athari za utandawazi pamoja na idadi ndogo ya watumiaji wa simu za mkononi ikilinganishwa na idadi ya watu waliyopo kwa sasa hapa nchini.
Mkurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA Prof. Jonh Nkoma amesema takwimu za sasa zinaonesha kuwa idadi ya watumiaji wa simu za mkononi wanafikia milioni 8 sawa na asilimia 20 ya watanzania.
|