|
Jeshi la polisi linahitaji msaada kupambana na ajali za barabarani
2008-05-11 19:50:02
Na ITV Habari
Jeshi la polisi limesema lipo tayari kushirikiana na taasisi yeyote ya umma na binafsi katika juhudi za kukabiliana na majanga ya ajali za barabarani zinazoongezeka na kupoteza maisha ya mamia ya watanzania.
Hayo yamesemwa na kamanda wa kikosi cha usalama barabarani kamishna masaidizi James Kombe wakati wa hafla ya kufunga na kukabidhi vyeti kwa maafisa wakaguzi wa jeshi la polisi mkoa wa Dar es Salaam.
Naye mwezeshaji wa mafunzo hayo Bw Said Seif amesema mafunzo hayo yatawawezesha polisi kuongeza ufanisi wa kukagua magari ili kupunguza ajali za barabarani.
|