|
Vijana wametakiwa kuiga mfano wa viongozi wa dini
2008-05-11 19:47:44
Na ITV Habari
Spika wa bunge la Jamhuri amewashauri vijana nchini kuiga mfano wa viongozi wao wa dini ilikuondoa tabaka za kijamii na kuimarisha amani, umoja na mshikamano uliopo mingoni mwa watanzania.
Mh. Sitta ametoa rai hiyo huko Urambo mashariki mkoani tabora kwenye ibada ya upadrisho iliyofanyika katika kanisa katoliki urambo.
Katika mahubiri yake askofu mkuu wajimbo kuu la Tabora mhashamu Paulo Lusoka amewataka viogozi wa dini kuzingatia mafundisho na maadili ya dini katika kuongoza waamini kwa mifano ya matendo mema.
|