|
Laston ateuliwa kuwa katibu mkuu katika wizara ya fedha na uchumi
2008-05-11 19:46:59
Na ITV Habari
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Laston T. Msongole kuwa naibu katibu mkuu katika wizara ya fedha na uchumi.
Taarifa iliyotolewa leo Ikulu, Dar es Salaam na katibu mkuu kiongozi, Bw. Philemon Luhanjo imesema uteuzi huo unaanza mara moja ambapo Bw. Msongole atashughulikia masuala ya uchumi na bajeti katika wizara hiyo.
Kabla ya uteuzi wake, Msongole alikuwa mkurugenzi wa masuala ya uchumi katika iliyokuwa wizara ya mipango, uchumi na uwezeshaji.
Wizara hiyo ilifutwa katika mabadiliko ya muundo mpya wa serikali uliotangazwa na Rais Kikwete Februari mwaka huu.
|