|
Waliounguliwa na nyumba mtaa wa Sikukuu bado hawajarejea
2008-05-11 19:45:55
Na ITV Habari
Wakazi waliokuwa wanaishi katika nyumba iliyoungua na kusababisha kuteketea kwa bidhaa katika eneo la Sikukuu karibu na msikiti wa Mtoro bado hawajarejea katika makazi yao.
Wamesema kuwa bado eneo hilo linafanyiwa uhakiki ili kujua chanzo cha moto huo ambao uliwaka kwa zaidi ya masaa kumi katika eneo la ghala na kusababisha hasara kubwa pamoja na kufanya tathmini itakayotoa taarifa ya gharama za bidhaa zilizoteketea katika moto huo.
|