10 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Mtwara na Lindi waomba wafugaji waendelea kuhamia kwao
 
2008-05-10 18:08:57
Na ITV Habari

Wadau wa mifugo wa mikoa ya Mtwara na Lindi wameiomba serikali, kuendelea kuwahamasisha wafugaji hasa wa ng`ombe, kupeleka mifugo yao mikoa ya Kusini, pia kuanzisha viwanda vya kusindika nyama ili kukuza biashara ya mifugo, kutokana na mikoa hiyo kuwa nyuma katika shughuli za ufugaji.

Wadau hao wametoa maombi hayo kwenye warsha iliyoandaliwa na wizara ya mifugo na uvuvi, yenye lengo la kuandaa mkakati wa kutekeleza sera ya taifa ya mifugo ya mwaka 2006 ambapo wamesema uchache wa mifugo na madawa ya kutibu maradhi, umesababisha bei ya nyama kwa walaji kuwa kubwa.

Hata hivyo mtaalamu wa kilimo toka chuo kikuu cha kilimo - SUA -cha Morogoro Prof. Lusato Kuligila amesema changamoto inayowakabili wafugaji wa mikoa ya kusini, ni upatikanaji wa mifugo bora na udhibiti wa magonjwa.

  • SOURCE: ITV
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.