|
Jumla ya silaha 53 zakamatwa mkoani Mbeya
2008-05-10 18:08:10
Na ITV Habari
Jumla ya silaha 53 zimekamatwa na zingine kusalimishwa mkoani Mbeya katika kipindi cha miezi mitatu baada ya jeshi la polisi kufanya msako wa matukio ya uhalifu katika mkoa huo.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya bwana Suleiman Kova amesema kuwa silaha hizo zilikamatwa wilaya za Mbozi, Mbarali, Kyela na Chunya na kwamba baadhi ya silaha hizo zimekamatwa nyumbani kwa watuhumiwa ambao tayari wamefikishwa mahakamani huku silaha zingine zikisalimishwa katika ofisi za watendaji wa vijiji.
|