|
Utafiti wa mafuta katika maeneo kadhaa yanaonyesha mafanikio kiasi
2008-05-09 12:17:55
Na ITV Habari
Shirika la maendeleo ya petroli TPDC limesema makampuni yanayoendelea na utafiti wa mafuta katika maeneo kadhaa yanaonyesha mafanikio kiasi kutokana na dalili za awali zinazoonyesha kuwepo kwa mafuta katika vina virefu vya bahari.
Hayo yameelezwa na mjiolojia mkuu wa mafuta kutoka TPDC Bwana Herry Kajato wakati akielezea jitihada za harakati za utafutaji wa mafuta na gesi zinazofanywa na makampuni kumi na tisa yaliyopewa vibali na TPDC kwa ajili ya kazi hiyo.
|