|
Pato la Mtanzania sasa ni dola 526 kwa mwaka
2008-05-08 14:34:52
Na ITV Habari
Pato la taifa kwa mwaka huu limeongezeka na kufikia trilioni 25 ukilinganisha na trilioni 21 zilizopatikana katika mwaka uliopita, na kufanya wastani wa pato la mtu kufikia dola 526 kwa mwaka.
Hayo yamesemwa na waziri wa fedha na uchumi Mh. Mustafa Mkulo wakati akizungumzia kukua kwa pato la taifa sawia na kuongezeka kwa ukuaji wa sekta mbalimbali zinazochangia uchumi wa nchi ikiwemo kilimo na uvuvi.
Aidha mh. Mkulo amesema michango ya shughuli za kiuchumi katika pato la taifa limechangiwa kwa kiasi kikubwa na sekta ya uvuvi, misitu na uwindaji kwa asilimia 45.5 kwa mwaka 2001 na asilimia 43.8 kwa mwaka 2006.
|