08 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Benki za biashara nchini zimetakiwa kusambaza huduma vijijini
 
2008-05-08 14:34:04
Na ITV Habari

Benki za biashara nchini zimetakiwa kuonesha kwa vitendo uwezo wake wa kupanua wigo wa huduma zao kwa watanzania kwa kupeleka huduma zao kwenye mikoa na wilaya na vijijini badala ya kung`ang`ania miji mikubwa yenye biashara na shughuli nyingi za kiuchumi.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bw. Yohana Balele amesema hayo wakati akizindua tawi la benki ya Posta mkoani humo ambapo mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo Bw. Alphonce Kihwele amesema uzinduzi huo ni katika mipango ya kusambaza huduma zake kuweza kufikia watanzania walio wengi zaidi.

  • SOURCE: ITV
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.