|
Serikali imewataka wajasiriamali nchini kuchangamkia fursa za utoaji mikop
2008-05-07 11:33:58
Na ITV Habari
Serikali imewataka wajasiriamali nchini kuchangamkia fursa za utoaji mikopo katika asasi za fedha ili kukuza mitaji itakayowawezesha kuleta ushindani katika soko la jumuiya ya Afrika Mashariki.
Changamoto hiyo imetolea na waziri wa viwanda, biashara na masoko Mh. Mary Nagu wakati akizungumza katika ufunguzi wa maonesho ya biashara kanda ya kaskazini yaliyofanyika katika viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la kuhudumia viwanda vidogo nchini - SIDO Bw. Mike Laizer amesema hivi sasa wadau wao wameanzisha muungano wa wajasiriamali vijijini -Muvi hasa kwa mkoa wa Tanga ambao utasimamiwa na wizara ya viwanda na baishara na masoko kwa lengo la kuwatafutia masoko ya kutosha.
|