|
Wanaotoa huduma kwa wawekezaji nchini wahakikisha wanatoa huduma kikamilifu
2008-05-07 11:33:35
Na ITV Habari
Mamlaka ya ukanda wa mauzo ya nje- EPZ imewataka wadau wanaotoa huduma kwa ajili ya wawekezaji nchini kuhakikisha wanatoa huduma kikamilifu na kuhakikisha kuwa wawekezaji wanaokuja kuwekeza hapa nchini hawapati usumbufu katika utoaji na usafirishaji wa mizigo yao
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa maendeleo ya uwekezaji kutoka EPZ zawadia nanyaro wakati alipokuwa akizungumzia changamoto wanazokabiliana nazo wawekezaji wanaokuja kuwekeza hapa nchini kwa ajili ya kuinua uchumi wa nchi.
|