|
Wanawake wachimbaji wametakiwa kujiimarisha katika umoja wao
2008-05-06 15:27:26
Na ITV Habari
Wanawake wachimba madini hapa nchini wametakiwa kuimarisha umoja wao pamoja na kutumia vikundi vyao kuomba mikopo mikubwa katika vyombo vya fedha ili waweze kuongeza ufanisi katika biashara zao ikiwemo kuyaboresha madini kabla ya kuyauza ili kuyaongezea thamani ili waweze kuyauza kwa bei ,nzuri zaidi.
Mke wa rais Mama Salma Kikwete amesema hayo katika maadhimisho ya siku ya wachimba madini hapa nchini iliyoandaliwa na chama cha wanawake wachimba madini hapa nchini -TAWOMA ambaye amewataka kujikita katika mafunzo zaidi ya ukataji na usanifu madini.
|