19 Mar 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Asilimia 98 ya dawa hazithibitishwi ubora wake kabla ya kuingia sokoni
 
2008-03-19 11:13:56
Na ITV Habari

Asilimia 98 ya dawa zinazotakiwa kuthibitishwa ubora wake kabla ya kuingia sokoni zimebainika kuwa na kemikali hatari za sumu zinazochangia kusababisha madhara makubwa kiafya.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam na katibu mkuu wizara ya afya na ustawi wa jamii, Bw. Wilson Mukama wakati akizundua kamati maalum ya kitafa ya kusimamia kemikali na kuwataka kutotoa vibali vya dawa hizo kuingia sokoni.

Wakitoa ufafanuzi wa utendaji kazi wa kamati hiyo itakayokuwa chini ya mkemia mkuu wa serikali, wakala wa usalama wa afya kazini Dk. Peter Riwa amesema kuna idadi kubwa ya kemikali za viwandani zinazozagaa katika maeneo ya makazi ya watu ambazo hazijahifadhi vizuri na hivyo kuhatarisha za afya za watu.

  • SOURCE: ITV
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.