|
TAG Kijitonyama wamefanya ibada ya kumwomba Mungu aipe serikali ujasiri
2008-02-25 16:16:54
Na ITV Habari
Waumini wa kanisa la Tanzania Assemblis of God - TAG Kijitonyama wamefanya ibada ya kumwomba Mungu aipe ujasiri serikali iwachukulie hatua mafisadi na kupunguza gharama za umeme .
Ibada hiyo iliyofanyika kwa muda wa masaa mawili ikiongozwa na mzee kiongozi wa kanisa hilao Bw. Deoglas Sallu ambaye amewataka viongozi wa dini kuacha ushabiki wa vyama na kutetea maslahi ya umma.
|