|
Timu ya wavulana ya mpira wa meza kutoka Malawi yaongoza
2008-02-02 11:38:14
By ITV Habari
Timu ya wavulana ya mpira wa meza kutoka Malawi imeendelea kuongoza katika mashindano ya wazi yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wa wanaume chini ya umri wa miaka 18, wachezaji Kingwel Kaunda na Abel Somba kutoka Malawi wamefikia hatua ya nusu fainali.
Ama kwa upande wa wasichana, waliofanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ni Afuweni Sam kutoka Malawi na Neema Mwisiyula kutoka Tanzania.
|