|
Serikali ya Kenya imekiri kuwa ukabila ni tatizo la kitaifa
2008-05-17 14:56:24
Na EAR Habari
Hatimae Serikali ya Kenya imekiri kuwa ukabila ni tatizo la kitaifa ambalo linahitaji juhidi za pamoja na za dhati ili kukabiliana nalo.
Mswaada uliochapishwa wiki hii wa kuanzishwa kwa kamisheni ya maadili ya taifa na mahusiano ya kitabaka ni matokeo ya kukubali kuwa ufumbuzi wa kuleta amani utapatikana pale tu kutakapokuwa na utayari wa fursa sawa kwa wote.
Mswaada huo unataka kuipa serikali mamlaka ya kushughulikia kikamilifu matukio mabaya ya kikabila ambayo yamekuwa yakijitokeza katika maeneo mengi nchini.
|