|
Theluthi 3 ya dawa za kutibu ugonjwa wa Maralia jiji la Kampala ni madawa bandia
2008-05-17 14:55:54
Na EAR Habari
Utafiti uliofanywa nchini Uganda unaonesha kuwa zaidi ya theruthi tatu ya dawa za kutibu ugonjwa wa Maralia katika jiji la Kampala ni madawa bandia au hazina nguvu ya kutosha utibu ugonjwa huo.
Kutokana na utumiaji wa madawa bandia au yasiyokuwa na nguvu wanasayanzi wameonya kuwa ugonjwa wa maralia unawewza kuwa sugu katika kizazi hiki cha madawa ambacho kimeleta dawa mbadala na kuiondoa chloroquine.
Utafiti huo unonesha kwamba asilimia 35 ya dawa ziliozofanyiwa uchunguzi zilikuwa bandia na nyingine zikiwa na ubora mdogo ukilinganisha na ubora unaohitajika.
Tafiti hiyo pia ilifanyika katika nchi za Ghana, Kenya, Nigeria, Rwanda,Kenya ikiongoza kwa kuwa na madawa yasiyona ubora kwa asilimia 38.
|