|
Kamishna Awounda wa Kenya ameshangazwa na miswaada kuchapishwa kwa siri
2008-05-16 15:32:36
Na EAR Habari
Kamisheni ya upatanisho haki na ukweli nchini Kenya TJRC imelezea wasiwasi kuwa huenda serikali ikatumia uwezo wake kuingilia kati shughuli ambazo zinafanywa na kamisheni hiyo.
Kamishina Gad Awounda alitoa tahadhali hiyo katika hafla iliyoandaliwa na kamisheni hiyo kwa umoja wa wahariri jijini Nairobi akielezea wasiwasi wa mswaada mpya wa kamisheni hiyo na ule wa kamisheni ya maadili ya kitaifa na mahusiano kitabaka.
Awounda amesema kuwa ameshangazwa na miswaada hiyo kuchapishwa kwa siri mnamo tarehe 9 mwezi may, ambao ungetakiwa kuwa mwanzo mpya kwa wakenya ambao wanateseka kwa kutopata haki,na akaainisha kama mianya haitashughulikiwa kutawagawa wakenya zaidi.
|