|
Ndoa za jinsia moja nchini Marekani ni kinyume cha katiba
2008-05-16 15:25:41
Na EAR Habari
Mahakama ya juu katika jimbo la California nchini Marekani imeamua kwamba sheria katika jimbo hilo inayyozuia ndoa ya jinsia moja kuwa ni kinyume cha katiba.
Mahakama hiyo katika uamuzi wake imesema kuwa haki ya kuanzisha uhusiano wa familia inawahusu wakazi wote wa jimbo hilo bila kujali jinsia zao.
Marufuku hiyo iliidhinishwa na wapika kura mwaka 2000 lakini ilipingwa na wanaharakati mashoga na mamlaka ya mji wa San Francisco, na mara mbili bunge jimboni humo liliruhusu ndoa ya mashoga lakini gavana wa jimbo hilo Arnold Schwarzenegger alitumia kura ya turufu kupinga.
|