16 Jul 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Tume ya uchaguzi Kenya yatoa agizo kwa jeshi la polisi
 
2006-07-16 19:01:12
Na EAR Habari

Tume ya Uchaguzi nchini Kenya imeliagiza jeshi la polisi nchini humo, kuwakamata na kuwashitaki watumishi wa umma, wanaowapigia kampeni baadhi ya wagombea, katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika julai 24 mwaka huu.

Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Gabriel Mukele, amesema kanuni za uendeshaji za uchaguzi zinaizuia serikali kutumia rasilimali za taifa kwa manufaa ya mgombea au chama chochote.

Amesema watumishi wa umma hawapaswi kushabikia upande wowote, hivyo tume hiyo itapambana vikali na mtumishi yeyote atakayekiuka sheria hiyo.

Uchaguzi huo mdogo utafanyika katika majimbo ya Nakuru Mjini, Laisamis, Horr Kaskazini, Saku na Moyale, kufuatia vifo vya wabunge watano, katika ajali ya ndege iliyotokea April 10 wilayani Marsabit.

  • SOURCE: EAR
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.