17 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Mfanyabiashara anayedaiwa kununua vitu vya wizi Mbeya atiwa mbaroni
 
2008-05-17 15:43:48
Na Mwandishi Wetu, Jijini

Mfanyabiashara Richard Komba, 32, mkazi wa Jijini Mbeya anashikiliwa na Polisi mkoani humo baada ya kudaiwa kupatikana na vitu kibao vya wizi uliotokea katika maeneo mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoani humo,Suleiman Kova, mtuhumiwa huyo ametiwa mbaroni kutokana na msako ulioendeshwa na jeshi lake kuanzia Mei 14 mwaka huu.

Akasema kutokana na msaada wa wananchi katika utekelezaji wa ulinzi shirikishi, wakaweza kumnasa mpokeaji huyo maarufu wa bidhaa za wizi, ambaye ni mkazi wa Mtaa wa BOT uliopo katika eneo la Forest Jijini humo.

Aidha, Kamanda Kova amesema watu kadhaa wanaotuhumiwa kwa uhalifu wa kuvunja majumba ya watu usiku na kupora vitu mbalimbali wamekamatwa na kutiwa mbaroni.

Kamanda Kova amewataja watu hao kuwa ni pamoja na Frank Mwamlima, 28, mkazi wa Majengo Jijini Mbeya, Kelvin Wilson, 21 aliye makzi wa Mabatini, Rashid Mkwale, 28 aliye mkazi wa Mabatini pia na Ephraim Edward, 28, mkazi wa Mbalizi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wengine ni Paulo Solo, 22 (mkazi wa Ivumwe), Jeco Daud, 20 (Isanga), Amran Mwilapa, 25 (Ilolo), Cosmas Sinyinza, 25 (Makunguro), Gallus Boniphace Mlema \'Baba Bony\', 34 (Block T), George Aron, 18 (Isanga), Jumanne Mpora, 26 (Makunguru) na Frank Edward, 28, mkazi wa Mbalizi.

Watuhumiwa wengine wa uhalifu ni Alunanuswa Mwalukasa, 34, ( Iyunga), Asifiwe Josiah, 24, Juma Magesa, 42, Zubeir Hamis, 30 (wote Isanga), Frank Manyanya, 30 (Mbalizi), Itika Mwasanguti, 38 (Mama John), Jackson Masebo, 25 (Nzovwe), Neza Christopher, 29 (Nzovwe), Shemu Simtore, 42, (Mambwe) na Emmanuel Michael, 24, mkazi wa Uyole.

Kamanda Kova amevitaja baadhi ya vitu ambavyo watuhumiwa hao wanadaiwa kuviiba kuwa ni pamoja na seti 19 za luninga za aina mbalimbali, redio nane, deki za DVD nne, spika tisa za redio, baiskeli mbili, amplifier moja aina ya Sansui na waya za TANESCO.

Akasema uchunguzi zaidi unaendelea na watuhumiwa hao watafikishwa kortini wakati wowote kuanzia sasa.

Hata hivyo, akasema Kamanda Kova kuwa hadi sasa wanaendelea na msako zaidi ili kumbaini mfanyabiashara mwingine ambaye hakumtaja jina, anayeelezewa kuwa naye ni kinara wa ununuzi wa vitu vya wizi.

Akawaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kila mara wanapohisi jambo linalowahatarishia usalama wao wenyewe na mali zao, ili hatimaye wahalifu wakamatwe na kufikishwa korini .

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.