|
Abambwa akimbaka mwanafunzi
2008-05-10 19:40:51
Na Kiyao Hoza, Polisi Kati
Mtu mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi Jijini baada ya kubambwa laivu akimbaka mtoto mwenye umri wa miaka 14. Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Faustne Shilogile amtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Nathan Msingwa, 20, mkazi wa Kitunda ambaye kazi yake imetajwa kuwa ni dereva.
Akifafanua tukio hilo, Kamanda Shilogile amesema tukio hilo limetokea jana asubuhi ambapo mtuhumiwa alibambwa laivu na wananchi wa eneo hilo, ambao baada ya kumfuma wakaamua kumshushia kipigo kikali kwa kutumia silaha mbalimbali za jadi.
Akasema kutokana na kipigo hicho, mtuhumiwa amejeruhiwa vibaya sehemu za kichwani na usoni.
Akasema msichana aliyefanyiwa unyama huo (Jina limehifadhiwa) hivi sasa yupo katika Hospitali ya Amana kwa matibabu na uchunguzi zaidi.
Hata hivyo, Kamanda Shilogile ametoa wito kwa wananchi kutochukua sheria mkononi na badala yake wanapowakamata wahalifu kama huyo wawapeleke kwenye vyombo husika kwa wajili ya kuchukuliwa hatua stahili za kisheria.
|