10 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wadau wa daladala kujikwamua kiuchumi
 
2008-05-10 19:38:11
Na Judith Francis, PST - Jijini

Chama cha Kuweka na Kukopa cha Daladala SACCOS kimetoa wito kwa madereva, makondakta, wamiliki wa mabasi na jamii kujiunga na chama hicho ili waweze kuweka na kukopa ikiwa ni njia mojawapo ya kuweza kujikwamua kiuchumi.

Rai hiyo imetolewa na Meneja Msaidizi wa chama hicho, Bw. Athumani Sururu, wakati alipokuwa akizungumza na PST Jijini jana.

Akasema lengo la kuanzisha chama chao hicho ni kusaidia madereva, makondakta, wamiliki wa magari na pia watu wengine wasio katika biashara za daladala ili waweze kuwekeza na kisha kupata mikopo kwa ajili ya kuendeleza biashara na shughuli nyingine zao nyingine za kiuchumi.

``Makundi kama haya ya watu wa daladala yanasahulika kwani wengi hawana pesa za kutosha na hawawezi kwenda kukopa benki kwa sababu mikopo yake ina riba kubwa... lakini sisi tunaweza,`` akasema.

PST ilipotaka kujua kwa nini chama hicho kimewakaribisha wamiliki wa mabasi ya abiria wakati lengo ni kuwasaidia wenye kipato cha chini, Bi. Rehema akasema wao hawana ubaguzi.

``Sheria haitaki ubaguzi kwenye vyama... pia kuna wamiliki wenye gari moja na hivyo wanahitaji kupata nguvu zaidi ya kuimarisha biashara zao,`` akasema.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.