10 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wakuu wa shule za sekondari nchini kujadili vurugu, migomo
 
2008-05-10 19:35:08
Na Haji Mbaruku, Jijini

Wakuu wa Shule mbalimbali nchini wamekutana Jijini kujadili vurugu, migogoro na migomo ya wanafunzi mashuleni ili kuweza kuyapatia ufumbuzi na yasiendelee kutokea.

Akizungumza na Alasiri, Mkuu wa shule ya Tambaza, Bw. Nicholaus Buleta amesema kuwa, wanatarajia michango ya walimu mbalimbali itatolewa ili kubaini chanzo cha migogoro hiyo.

Wakuu hao wa shule za sekondari wanakutana kufuatia kuzuka kwa vurugu katika shule mbalimbali hapa nchini.

Katika tukio la hivi karibuni, wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kantalamba iliyopo mkoani Rukwa walifanya vurugu shuleni hapo na kuutupia lawama uongozi wa shule hiyo kwa kushindwa kuiendesha shule hiyo vizuri.

Vurugu hizo zilisababisha kutokea kwa hasara kubwa kutokana na uharibifu mkubwa unaodaiwa kusababishwa na wanafunzi hao.

Katika vurugu hizo, uongozi wa shule hiyo umeamua kuifunga shule hiyo na kuamuru wanafunzi wake kurudi majumbani kwao hadi watakapotangaziwa tena.

Vurugu nyingine zilitokea huko Mbeya ambayo wanafunzi wa shule moja nao walilazimika kufanya vurugu na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali za shule hiyo.

Hata hivyo, Bw.Buleta ambaye pia ni Rais wa umoja wa wakuu wa shule za sekondari nchini, amesisitiza kuwa mkutano huo utalenga kupata suluhisho la kudumu la tatizo la vurugu kwenye shule zao za sekondari.

Naye, Naibu waziri wa Elimu, Bi.Mwantumu Mahiza amekaririwa akiwataka wakuu wa shule za sekondari nchini kujiangalia upya, wajifikirie, wajikague na wajiulize kwanini vurugu zimevuka mipaka mashuleni.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.