09 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Tabata Dampo, balaa tupu!
 
2008-05-09 19:21:44
Na Job Ndomba, Tabata Dampo

Wakazi kadhaa wa eneo la Tabata Dampo, Ilala Jijini waliobolewa nyumba zao, wameapa kupambana vikali iwapo mtu yeyote atatia pua yake hapo leo kwa lengo la kuwahamisha kwa nguvu.

Wakizungumza na Alasiri ilipotembelea eneo hilo leo asubuhi, wakazi hao wamedai kuwa, wamendaa silaha za jadi yakiwemo mapanga, mishale, visu na virungu kwa ajili ya mpambano huo kama mmoja wa wahanga hao anavyoonekana pichani ukurasa wa mbele kulia.

Wamesema wamefanya maandalizi hayo, baada ya kampuni inayodai kumiliki eneo hilo ya Allied Frieght Cargo Ltd kuwapa saa 24 kuhakikisha wameondoka kwa hiari yao ama sivyo wataondolewa kwa nguvu.

Imeeelezwa kuwa wananchi hao wamejipanga kikamilifu toka mishale ya alfajiri baada ya kutonywa na watu kuwa, \"wabaya wao\" kama wanavyodai wangefika katika eneo hilo asubuhi na mapema kwa ajili ya kutekeleza zoezi hilo la kuwahamisha.

Akizungumza na Alasiri, msemaji wa wahanga wa eneo hilo, Bw. Tauzan Hariri Mbwana, amesema hawako tayari kuondoka hadi pale mahakama itakapotoa uamuzi wake.

Amedai kuwa kilichoawatia hasira zaidi ni vitisho vilivyotolewa na mmiliki wa kampuni hiyo na kwamba tayari wamekwishaongea na mwanasheria wao ili waweze kufungua kesi nyingine zaidi mahakamani.

Wameongeza kuwa hata eneo la Buyuni wanalotakiwa kuhamia na kuweka makazi mapya, bado hawajapewa viwanja na wanashangaa wanataka kuwatimua ili waende wapi.

Februari 29 mwaka huu nyumba 88 zilizojengwa katika eneo hilo zilibomolewa na Manispaa ya Ilala na kusababisha takribani zaidi ya familia 300 kukosa makazi.

Baadaye Serikali ilipinga zoezi la ubomoaji wa nyumba hizo na kudai lilikuwa limetendwa kinyume cha Sheria baada ya Tume iliyounda na Serikali kubaini ukiukwaji wa hali ya juu wa sheria zilizotumika kusimamia zoezi hilo.

Kutokana na hilo, Serikali iliahidi kuwalipa wahanga wa tukio hilo fidia ya milioni 20 kila mmiliki wa nyumba katika eneo hilo, ambapo wakazi hao walikabidhiwa hundi zao za malipo wiki iliyopita.

  • SOURCE: Alasiri
Tuma Maoni Yako
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.