|
Dodoma yapeta
2008-05-08 14:42:36
Na Azizi Issa
Mkoa wa Dodoma umevuna lengo la uzalishaji kwa asilimia 100 baada ya kubuna tani milioni 1.2 za mazao ya chakula.
Mkuu wa mkoa huo, William Lukuvi, amesema kuwa kiwango hicho ni kile kilichozalishwa mwaka jana.
Aidha, akasema mwishoni mwa mwaka huu kutakuwa na upungufu mkubwa wa chakula nchini.
Akawataka wananchi mkoani humo kutumia kwa uangalifu chakula watakachovuna ili kuepuka uwezekanao wa kukabiliwa na upungufu wa chakula.
Pia akawataka kujenga tabia ya kufanya kazi kwa bidii na kuacha uvivu.
Akasema hilo litasaidia katika kuleta maendeleo ya haraka katika jamii na Taifa kwa ujumla.
|